TANZANIA: Idea ya wimbo inaendana na maisha yangu - Pipi

 

 

Msanii wa muziki, Pipi amesema wimbo wake mpya ‘Hafai’ aliyomshirikisha Nick wa Pili ameuandika kwa miaka 3.

Muimbaji huyo ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu, ameiambia Bongo5 kuwa muda wote ambao alikuwa kimya alikuwa anawaandalia muziki mzuri mashabiki wake.

“Idea ya wimbo inaendana na maisha yangu, nafanya kazi ya muziki pia naishi maisha yangu, yaani idea ilikuja automatic kutokana na life style yangu,” alisema Pipi. “Kwa hiyo ni wimbo ambao idea yake ilikuja kutokana na aina fulani ya maisha ambayo vijana wanaishi, wanaona wapo sawa lakini sio sawa. Sio kila kitu katika maisha kinacholeta furaha kinanunuliwa na pesa, nimezungumzia familia, watoto na ndoa,”

Aliongeza, “Wakati naandika huu wimbo sikufikiria kumshirikisha mtu, lakini kwa sababu ni wimbo ambao nimeanza kuuandika tangu 2013, ni miaka 3 mpaka sasa, idea zikawa zinaongezeka, ndo nikaona nimshirikisha Nick wa Pili, hata hivyo mambo yamekuwa mazuri,”

 

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment