TANZANIA: Sina bahati -Steve Rn’B

 

Msanii wa RnB Steve amefunguka na kutufahamisha kuwa alifunga ndoa na hakuwa na bahati kwenye ndoa yake hiyo ambayo kwa sasa imevunjika na kusema sababu za kuvunjika kwa ndoa hiyo ni maneno maneno tu amabayo hawezi kuyaelezea.

Pia Steve amesema alifanikiwa kupata mtoto mmoja katika ndoa yake na kusema ndoa ni kati ya watu wawili hivyo makubaliano ya kuachana yalikuja baina yao na pia itakapofikia wakati wa kurudiana wataamua wao.

Steve amesema anatarajia kuachia ngoma yake mpya ambayo amemshirikisha Bill Nass na kusema ndani ya ngoma hiyo watu watarajie kupata ladha na ubunifu kama ilivyo kawaida yake akidai kuwa huwa hakosei anapoamua kuachia ngoma.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment