TANZANIA: "Mashabiki zangu wapo wawazi kwangu" - Belle9

Mwanamuziki wa Bongo fleva ashambuliwa na mashabiki baada ya kubadili staili ya nywele. Akizungumza na Enewz Belle 9 alisema kuwa msanii yeyote ambae anaijua sana siku zote huwa hana mipaka na kazi yake anaweza akafanya kitu chochote kuhusiana na sanaa yake hivyo hata yeye hana mipaka kwani rangi hiyo aliyoiweka katika nywele ''brichi'' zake inamaana ya thamani ya mtu mweusi .

“Style tofauti tofauti za nywele mimi nilianza kuweka muda mrefu tangu sijaanza kufanya mziki mimi nilikuwa hadi nikisuka na hii rangi yangu ni nyeusi na kichwani nina gold nikiwa ninamaanisha watu weusi tunathamani maana nimekuwa nikiona watu weusi sehemu tofauti tofauti wakidharauliwa na kubaguliwa,

"Mimi nimependa vile kwasababu kuna watu katika mitandao ya kijamii wao kila kitu wanaona sawa na nashukuru kuona watu kwa mara ya kwanza wamepinga ambacho mimi nimefanya,mimi ninamashabiki wazuri kumbe nikifanya kitu wanaweza kunielimisha wapo huru na mimi hawanihofii yaani mashabiki zangu wapo wawazi kwangu”,alisema Belle 9.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment