TANZANIA: Mimi sifanyi muziki kama fasheni - Darasa

 

Pamoja na kufanikiwa kuliteka soko la muziki Bongo kupitia ngoma hiyo rapa huyo anaetamba bado kupitia kibao hicho mpaka sasa wanadai kuwa hajafanya show yeyote ya ngoma hiyo kitu ambacho kinawashangaza wadau wengi wa muziki.

Akizunguma na Enew Darasa alisema kuwa yeye anafanya show nyingi sana sema watu hawajui tu pia si lazima kila anachofanya watu watambue kwasababu yeye si mtu wa showoff na anataka atambulike kupitia kazi zake na wala si kwa kiki ama chochote kile tofauti na kazi.

"Sisi hatupo kwakutegemea kitu kimoja tuna vitu vingi tunavifanya na hatuhitaji kufanya haraka tunahitaji muda na tunahitaji kufanya kazi mimi sifanyi mziki kama fasheni ni mtu ambae natengeneza mipango ya kesho na keshokutwa ili hata nisipoimba mimi basi basi aje aimbe mtu ambae hata wewe ukimsikia uwe unasema ameimba kwasababu Darasa yupo nina mipango mikubwa ya kufanya ya kuendelea leo na kesho",alisema Darasa.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment

Other news