TANZANIA: Sisi wasanii maisha yetu wengi ni feki tunavyoonyesha kwenye Instagram – Nikki wa Pili

Msanii Nikki wa Pili amefungukia maisha ya wasanii wa bongo ambayo yeye ameyaita ni feki na kashfa. Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Nikki wa Pili amesema wao ni watu ambao jamii wanawaangalia kama mifano kwao, lakini matokeo yake maisha ya uongo wanayoishi ndiyo ambayo jamii huyapokea hususan vijana.

“Sisi watu maarufu wasanii waigizaji ni watu ambao tunaonekana ni kioo cha jamii, ni role model, ni mfano wa kuigwa, lakini mimi nimejaribu kuangalia hivi kweli sisi ni watu role model? Na jamii kama wanatuiga sisi wanaiga vitu sahihi!? Kwa mfano sisi wasanii maisha yetu wengi ni feki tunavyoonyesha kwenye instagram, tunayosema kwenye media sio vitu vya kweli, alafu vijana wanatuiga, itakuwa mapokeo gani kwenye jamii? Saa kama vijana wanaiga vitu feki kutakuwa na matokeo gani kwenye jamii?, alisema Nikki wa Pili.

Pia Nikki wa Pili aliendelea kuyasema haya juu ya maisha ya wasanii hao....... “Ukiongelea skendo za mjini ni za kwetu sisi wasanii, kashfa za vilevi za nini za kwetu wasanii, maisha ya uongo, kwa mfano msanii hawezi kupost picha instagram kama hajavaa nguo mpya”.

Kauli hiyo imefuatia baada ya kutangaza kuachia wimbo wake mpya unaoitwa 'role model' na jinsi alivyohusisha uhalisia wa maisha ya wasanii na wanachokipokea jamii.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

Leave your comment