TANZANIA: Wema Sepetu aonyesha uzalendo kwa kumuombea kura Diamond

 

Baada ya hivi karibuni Alikiba kuwaomba watanzania wampigie kura Diamond anayewania tuzo za BET, Wema Sepetu naye amefanya hivyo.

Wema ametumia mtandao wa Instagram kuwaambia mashabiki wake wampigie kura ex wake huyo aliyetajwa kuwania kipengele cha Best International Act: Africa.

“Uzalendo ndo unaotakiwa… Tanzania Kwanza Vingine Baadae… Ama nene…? Vote Vote Vote….,” ameandika Wema kwenye picha ya BET Awards aliyoiweka Instagram.

Mashabiki wengi wamempongeza kwa uzalendo huo aliounesha licha ya yeye na Diamond kuwa mbali kwa sasa kutokana na kila mmoja kuwa na maisha yake. Wema na mpenzi wa sasa wa Diamond kuwa na tofauti

Diamond anachuana na mastaa wengine wa Afrika wakiwemo Wizkid, Yemi Alade, AKA, Cassper Nyovest na wengine wawili.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

 

Leave your comment