TANZANIA: Tarehe 26 mwezi huu natarajia kuzindua kampuni yangu - Shetta

 

Msanii Shetta amesema hivi karibuni anatarajia kuzindua kampuni yake ambayo itahusika na kazi zake za muziki, pamoja na logo rasmi itakayomtambulisha.

Shetta ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha PlanetBongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwa sasa amepata uongozi mzuri unaomsimamia, ambao atauweka wazi siku ambayo atazindua kampuni yake.

“Tarehe 26 mwezi huu natarajia kuzindua kampuni yangu unajua, pamoja na logo, pia nitakuwa na Dj wangu official, na hata uongozi wangu mtaujua siku hiyo”, alisema sShetta.

Shetta ambaye kwa sasa anahit kwa wimbo wake mpya wa namjua, amewaahidi mashabiki wake wasiwe na wasi wasi kwani anakuja kivingine kabisa, tofauti na yule waliyemzoea, kutokana na uongozi huo mpya.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment