TANZANIA: Shamsa Ford akanusha kurudiana na Nay wa Mitego

Staa wa filamu Tanzania Shamsa Ford amesafisha hewa baada ya kuwepo kwa uvumi wa yeye na Nay wa Mitego kutamaniana kurudisha penzi lao.
Mwanamuziki wa Hip Hop Nay wa Mitego akiwa na muigizaji wa Bongo fleva Shamsa Ford.

Shamsa alifunguka yote hayo baada ya vyombo kadhaa vya habari na mitandao tofauti tofuti ya kijamii kuripoti kuwa Nay katika moja ya mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni alisema kuwa anatamani kurudiana na Shamsa Ford, kisha baadae ikadaiwa kuwa Shamsa naye amesema yuko tayari kurudiana na Nay, Shamsa alikanusha vikali uvumi huu.


Akizungumza na eNewz Shamsa alisema kuwa “Mimi siwezi kurudiana na Nay na kwasasa nina mpenzi wangu ninayempenda, kwahiyo Nay aendelee tu na maisha yake asitake kuniharibia mahusiano yangu, lakini kwa kuendelea kunisifu kwa mazuri hata baada ya kuachana, ninamshukuru na ninafurahi kwa hilo, lakini si zaidi ya hapo”.

 

Leave your comment

Other news