TANZANIA: “Mama ndiye aliyetambua kipaji changu” – Msami

 

 

Wimbo wa mabawa ni moja kati ya nyimbo zinazofanya vizuri katika media mbalimbali za hapa nchini na kubwa zaidi ni aina ya uchezaji wa wimbo huo. Hitmaker wa ‘Sound Track’ , ‘Mabawa’ ni miongoni mwa wasanii wachache hapa bongo wenye uwezo wa kuimb na kucheza kwa wakati mmoja. Msami ni msanii anayefany vizuri lakini hana mambo makuu.

Akiongea kwenye story tatu ya Planet Bongo inayorushwa na kituo cha East Afrika Radio, Msami alisema “Mama yangu ndiye mtu aliyetambua kipaji changu”. “Wakati niko mdogo nilikuwa napenda sana kucheza muziki, hata nilipokuwa nakataa kula walikuwa wanatafuta kanda ya muziki wananiwekea ndio hapo nitaweza kula”, aliongeza Msami

Kama ulipitwa na video ya ‘Mabawa’ ya Msami, hii hapa:

 

Chanzo: Bongo5.com

 

 

 

 

Leave your comment