TANZANIA: Rosa Ree ndani ya "The Industry"

 

 

 

Wanamziki Nahreel na Aika wa Navykenzo Wamemtambulisha rasmi msanii mpya ambae atakuwa chini ya lebel yao inayojulikana The Industry, Msanii huyu mpya ni Rapper wa Kike anayejulikana kama Rosa Ree....

 

Rose Ree

 Navykenzo Wameandika Kwenye Page yao hivi: Navykenzoofficial- Stoop!!! Anaitwa @rosa_ree ni rapper anaeletwa kwenu na mtayarishaji mahili na mmiliki wa studio @theindustrytz michael jordan wa beats @nahreel tunaomba mumpokee kwa mikono miwili kwasababu anajua pia kaeni mkao wa kula hivi karibuni mtaanza kumsikia masikioni mwenu..... #AboveInAMinute #GameGame #GoodMusicFamily

 

 

 

 

THE INDUSTRY MUSIC LABEL

 

TAARIFA KWA UMMA

 

UTAMBULISHO WA MWANAMUZIKI MPYA WA STUDIO YA MUZIKI YA “THE INDUSTRY”

 

Uongozi wa Studio ya Muziki ya The Industry iliyoko chini ya Wanamuziki Producer Nahreel na Aika Marealle unapenda kuchukua Nafasi hii kuwatangazia Umma Kuwa kuanzia Tarehe 14 January 2016 Wamemuingiza Msanii mpya wa Kike aitwaye Rosa Ree, Rose Ree ni muimbaji wa Muziki aina ya Rap ambae kazi zake zitaanza kusikika/Kuonekana siku si nyingi kuanzia sasa katika Redio Mbali mbali na TV Stations za Tanzania na nje ya nchi.

 

Kama wasikilizaji na watazamani tunaomba Kumuunga mkono Msanii huyu mpya Kwani tuna uhakika hatawaangusha katika kuwaletea burudani Katika Masikio na macho yenu pindi kazi zake zitakapoanza kutolewa hivi karibuni. Instagram anajulikana kwa jina la @rosa_ree

 

The Industry ni studio na kampuni ya muziki ambayo ipo chini ya kundi la music lenye Mafanikio makubwa la Navy Kenzo ikisimamiwa na Producer Nahreel na msaidizi wake Aika Marealle

 

Wasanii Baadhi Waliokwisha fanya kazi na Studio ya The Industry mpaka sasa toka kuanzishwa kwake hivi karibuni ni Diamond Platnumz na wimbo wake wa Nana, Nikki wa Pili na wimbo wa Baba Swalehe, Joh Makini na nyimbo zake kama Don’t Bother na nusu nusu.

 

Imetolewa na,

The Industry PR

John Kiandika.

 

 

Chanzo: UdakuSpecial.com

 

 

 

Leave your comment