TANZANIA: Diamond amtumia Idris salamu za Birthday bila kinyongo!

Msanii Diamond Platnumz ameonyesha kuwa hana bifu na Idris Sultan ambaye kwa sasa ni mpenzi wa ex wake, Wema Sepetu na kumtumia salamu za birthday katika ukurasa wake wa Instagram.

Diamond amemtumia Idris salamu za pongezi kwenye siku yake ya kuzaliwa Alhamisi hii. Hatua hiyo imekuja wakati amabo kila mtu alidhani Diamond na Idris haziivi tena kutokana na mshindi huyo wa Big Brother 2014 amepokea kijiti toka kwake.

Cha kushangaza zaidi hive karibuni Wema Sepetu na Baby mama wa Diamodn Zari walirushiana maneno ya kashfa mtandaoni.

Diamond aliweka picha ya Idris na kuandika maneno haya;

“Mtoto wa Mzee Sultan Leo Amezaliwa…. Now let’s All drop Our wishes Abi! @idrissultan”.

Leave your comment