TANZANIA: Linex adai huwa hafanyi vitu kwa kufuata mkumbo!

 

Linex amesema hafuati mkumbo wa kwenda kushoot video Afrika Kusini ndio maana ameamua kushoot video ya wimbo wake mpya ‘Kwa Hela’ Moshi na Arusha.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Redio Alhamisi hii, Linex amesema bado ana imani Tanzania ina kila kitu ambacho kinaweza kuzifanya video zake ziwe kali.

“Mimi sipendi kufanya vitu kwa kufuata mkumbo”, alisema. “Mimi napenda kufanya kitu kwa idea yangu ya jambo fulani, sifanyi kitu kwasababu fulani kafanya ndio maana sijaenda kushoot South Africa nimeshoot hapa, Moshi na Arusha”.

Aliongeza kuwa “Video itakuwa poa kwasbabu director nimempa kile alichotaka. Kwahiyo kila alichokiulizia director alipata, mimi nina imani kazi itakuwa poa kama tulivyotarajia”.

Leave your comment