TANZANIA: Siyo lazima kufanya kolabo na msanii wa nje ndio iwe hit song – AY

 

Msanii Ambwene Yesaya aka AY amesema siyo lazima ufanye kolabo na msanii kutoka nje ya nchi ndipo wimbo wako ufanye vizuri.

Msanii huyo ameyasema hayo baada ya kufanya remix ya wimbo wake wa ‘Zigo’ akiwa amemshirikisha Diamond Platnumz. Amesema amefanya hivyo kuwaonyesha wasanii wa ndani kuwa wanaweza kufanya kolabo za wenyewe kwa wenyewe na kwenda kimataifa.

“Dhana kubwa ya kufanya na ‘artist’ mwenzangu wa nyumbani ni kuonyesha kuwa tunaweza kutengeneza wimbo mkubwa na ukafanya vizuri bila kumtumia artist wan je”, AY aliiambia XXL ya Clouds FM hivi karibuni.

“Hii itasaidia sana kuchange mind za wasanii wenzangu . Haikatazwi ama kupingwa kufanya na artist wa nje but ‘we wanna show them’ kuwa industry yetu imekuwa kubwa sana, so cha msingi tuunganishe nguvu pamoja”’ alisisitiza.

Hadi sasa video ya wimbo wa Zigo Remix imefikisha views 450k kwenye YouTube.

 

Leave your comment