Nikki Mbishi Aja na "TOAST TO LIFE" Featuring Vanessa Mdee and Collo.

TOAST TO LIFE ni wimbo niliyoufanya takribani miaka mitatu iliyopita yaani 2013,kipindi Collo alikuja Tanzania.
Collo alipokuja Bongo alikuta wimbo wangu wa A.K.A unafanya vizuri akawish tukutane ndipo Dunga akatukutanisha na kufanya kazi hiyo.
Wazo la kufanya na Vanessa nilikuwa nalo kwa kuwa ni msanii mzuri na mpya hiyo angeweza kuweka taste ya kisasa zaidi na kufanya wimbo kuwa bora.
Mpaka sasa naweza kusema TOAST TO LIFE ni collabo kali kuwahi kutoka kwa kipindi cha hivi karibuni,hivyo naomba wafuasi wangu waipe support wakati niko chimbo nasaka madini mapya kama Videos na mazaga mengine.
Unju Bin Unuq.

Leave your comment

Other news