EXCLUSIVE (TANZANIA) – Wakazi, Diamond, Vanessa, Yamoto na Mpoto kutajwa kuwania tuzo za KORA AWARDS 2016

 

 

Tuzo za Kora Awards zimetangaza rasmi jana Disemba 3 majina ya wasanii wanaowania tuzo hizo, ambapo Tanzania inawakilishwa na wasanii watano.

Wakazi ametajwa kuwania katika kipengele cha Best Hip Hop, huku Diamond akitajwa kuwania kipengele cha Best Male East Africa, Vanessa Mdee akiwania Best Female- East Africa. Na Yamoto Band wakiwania kipengele cha Most Promising Male Artists of Africa, na bila kumsahau Mrisho Mpoto anayewania kipengele cha Best Traditional Male Artists of Africa.

Ambapo mbali na tuzo hizo zawadi kubwa ya mwaka huu ni kwenye kipengele cha Best Artist of The Continent itakuwa ni 1,000,000$ US dolla ambayo ni sawa na billioni 2.

Washindi wa vipengele vya Best Male Artists – West Africa, Best Female Artist- West Africa, Best Male Artist - East Africa, Best Female Artist – East Africa, Best Male Artist – Central Africa, Best Female Artist – Central Africa, Best Male Artist – Southern Africa, Best Female Artist – Southern Africa, Best Male Artist – North Africa na Best Female Artist – North Africa watapata 50,000$ sawa na zaidi ya shilingi milioni 100 kila mmoja.

Washindi wa vipengele vyote vilivyobaki watapata zawadi ya 20,000$ USD sawa na zaidi ya shilingi milioni 43 kila mmoja.

Hapo mwanzo tuzo za Kora zilipangwa kufanyika Disemba 13, 2015 Namibia na mwisho wa kupokea maombi ya wasanii waliotaka kushiriki ilikuwa ni Julai 20, 2015.

Tuzo hizo kwa sasa zitatolewa March 20, 2016 huko Windhoek, Namibia.

Hivi ni picha za vipengele vya wasanii wa Tanzania wanavyowania;

Leave your comment