EXCLUSIVE (TANZANIA): Mabeste Kumtumia Mke Wake Katika Video Zake Zote Zinazokuja

Rapper Mabeste asema baada ya kumtumia mke wake Lisa katika video yake ya “Usiwe bubu” na kufanya vizuri, ataendelea kufanya hivyo katika video zake zote zinazofuata. Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha EATV, alisema hata kikitokea kipengele cha ujambazi bado mke wake atacheza nafasi hiyo.Mabeste alisema “Hakuna video itakayotoka bila mke wangu Lisa, hata director akisema mnatakiwa kuiba benki tutaiba wote”

SIDEBAR

 CHARTS (TANZANIA): Hawa Ndio Wasanii 10 Wanaochezwa Sana Tanzania!

Pia aliongeza kuwa wameamua kumuingiza mtoto wao kwenye maswala ya Sanaa ili kumkuza kibiashara pamoja na kumwekea fedha zake zinazotokana na kazi hiyo ili kuweza kumsaidia katika maisha yake ya baadae.

RELATED 

 EXCLUSIVE(TZ): ''Sio picha nzuri mwanangu apatane na picha ya babake anamtia denda demu... '' Diamond Shares How Tiffa Has Changed His Life

Leave your comment

Other news