TANZANIA: Umapepe Nishautupa Kuleee! – Ruby

Hakuna asiyefahamu uwezo mkubwa wa muimbaji Ruby, lakini kila mmoja amekuwa akishangaa ni kwanini mrembo huyo anashindwa kwenda mbele zaidi kimuziki kutokana na kipaji chake cha asili kilichopo ndani yake.

Mrembo huyo ambaye ni zao la Serengeti Super Nyota 2014, aliwahi kufanya kazi na THT chini ya Ruge Mutahaba wa Clouds Media na kupata mafanikio makubwa sana kwa muda mfupi kupitia wimbo wake ‘Na Yule’ambao uliteka vyombo vya habari.

Hata hivyo hakukaa muda mrefu aliachana na uongozi huo kwa kashfa nyingi na kuamua kujisimamia mwenyewe lakini hakuweza kufanikiwa kwani kila siku zilivyozidi kwenda aliendelea kupotea taratibu huku mashabiki wakijiuliza kitu gani kinamsumbua binti hiyo.

Mwezi huu amerudi umpya na wimbo ‘Niwaze’ ambao unaonekana kuwavutia watu wengi huku wadau wakidai huwenda pia ni kutokana na ukimya wake wa muda mrefu.

Jumatatu hii mrembo huyo amedai ameachana na ‘umapepe’ kitu ambacho kilikuwa kikitajwa na watu wengi hasahasa wadau wa muziki kwamba ndio kinachomkwamisha mrembo huyo.

“Umapepe nishatupa kuleeekuleee tangu enzi za….niambie na ww mstari upi unakubamba,” Ruby alitoa ujumbe huo kupitia Instagram.

Kwa sasa muimbaji huyo hajaweka wazi anafanya kazi chini ya label gani lakini aliahidi mambo yakikaa sawa ataweka wazi kila kitu.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news