TANZANIA: Ujumbe Mzito Wa RAY C Kwa Marafiki Zake

Staa mkongwe katika game ya muziki nchini Rehema Chalamila maaraufu kama “Ray C” ameamua kutoa ushauri kwa jamii kuhusu marafiki ambao wamejaa usaliti na kuwataka wakae mbali na kuwalinganisha na nyoka ambao mbele ya macho yako hujifanya wazuri wakati nyuma ni wabaya wako.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Ray C ameandika ujumbe huo nakusema

“Ukiona rafiki kakugeuka usije thubutu kuwa nae karibu tena huyo ni zaidi ya nyoka tena bora nyoka ukikutana naye harembi kujifanyisha mzuri kwako anakugonga tu fasta kabla hujamdhuru kuliko anayejifanya kwako mzuri ukigeuka anakun’gon’ga Rafiki Mashwain kibao mjini!☠

Leave your comment

Other news