TANZANIA: Billnass Ajibu Tuhuma Zake

Rapa Billnass ambaye anatamba na ngoma ya 'Sina Jambo' amesema kupotea kwake katika 'game' ya muziki hakumaanishi kwamba ameshuka kisanaa kama watu wanavyodai kwa kuwa hajatoa ngoma yoyote kwa sasa ambayo ikashindwa kufanya vizuri.

Billnass amebainisha hayo kupitia eNewz ya EATV baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa ukimya wake umesababishwa na kuondoka kwa Petty Man katika 'label' ya LFLG na kumfanya msanii huyo kushindwa kujisimamia mwenyewe kazi zake.

“Huwezi kuzungumzia kushuka au kupanda kwa sababu bado sijatoa wimbo na 'fan base' yangu ni ile ile angalau ningekuwa nimetoa nyimbo zinakataa. Watu wanatoa nyimbo hata saba, nane, tisa zinakataa mimi sijatoa hata wimbo mmoja ukakataa kwa hiyo bado naamini 'material' ambayo ninayo ni mengi,” amesema Billnass.

Source: eatv.tv

Leave your comment

Other news