TANZANIA: Fid Q Aeleza Sababu ya Kuweka Wazi Mahusiano Yake Kwa Sasa

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Fid Q ameeleza ni kwanini sasa hivi ameamua kuweka wazi mahusiano yake ya kimapenzi tofauti na hapo awali.

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Fresh’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa kwa sasa amempata mtu ambaye wanaendana sawa kimtazamo hasa katika maongezi yao.

“Sikuwa na hiyo picha kwamba nakuja kuwa wa kwake, sema nilikuwa navutiwa na maongezi yake, yaani naongea na mtu ambaye anajua vitu vingi ambayo na mimi navijua,” amesema Fid Q.

“Unajua kuna vitu fulani unakuwa unaongea na watu, kuna watu wanakuwa wanakuona kama chizi na kuna mtu mwingine ikitokea unaongea naye na anakuelewa, labda vitu vya kisaikolojia na anakuelewa unaona inanoga, kwa hiyo hicho ndio kitu kilivutia zaidi,” ameongeza.

Rapper huyo ameongeza kuwa baada ya mazungumzo ya hapa na pale na mrembo huyo amegundua kuwa wapishana siku moja katika kuzaliwa (birthday), Fid Q amezaliwa, August 13 na mpenzie August 14.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news