TANZANIA: JK Awapa Neno Zito Wasanii

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni kipenzi cha wasanii, Jakaya Mrisho Kikwete, amewataka wasanii kufanya kazi zenye ubora zaidi ili kuweza kushindana na soko la kimataifa, la sivyo watabaki hapa hapa bongo.

Jakaya Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye ghfala ya uzinduzi wa Television Mpya ya Jason ambayo itakuwa inaonyesha filamu za kitanzania, na kusema kwamba ni wakati muafaka sasa kwa wasanii kuacha kulia lia kutaka serikali iwape msadaa, na badala yake wafanye kazi zenye ubora zaidi.

“Kama anavyosema Waziri isiwe sasa scene' ni hizo hizo tu, msilalamike tulindeni, mtabaki kibongo bongo tu, nyinyi mkitaka mtoke lazima muende beyond bongo, lazima muwe na product nzuri, na product nzuri mnaipata mkiacha ushindani, muhimu ni kusaidiwa mshindane vizuri, basi”, amesema Jakaya Kikwete.

Pamoja na hayo Jakaya Kiwete amesema amefurahishwa na muenendo wa tasnia ya sanaa ya filamu, ambayo kwa sasa imetoa ajira kwa watu milioni 6.

Source: eatv.tv

Leave your comment

Other news