TANZANIA: Alikiba Aeleza Umuhimu wa Elimu kwa Msanii, ‘Achana na Wanaoimba Ujinga’

Hitmaker wa ngoma Seduce Me Alikiba amezungumzia umuhimu wa msanii kuwa na elimu.

“Unajua ubongo wako ukiwa active utaweza kufikiria vitu vya msingi zaidi, achana na watu wanaoimba ujinga, ni kwa sababu tu ya talent lakini elimu ni ya muhimu sana kwenye kila kitu,” amesema Alikiba.

Katika mahojiano na Bongo5 ameeleza kuwa msanii akiwa na elimu kutamfanya kuweza kufikiri kwa undani zaidi na kumfanya yule anayemsikiliza kutambua msanii husika ni wa namna gani.

“Ukiwa na elimu kama wewe ni msanii ni rahisi kuonyesha watu ubongo wako ukoje, kwa sababu mkasa na visa vipo na maneno yapo lakini utamfanya mtu afikirie huyu alifikiria nini” amesema.

Alikiba bado anafanya vizuri na ngoma Seduce Me ambayo hadi kufikia sasa inaviews milioni 6.9 katika mtandao wa YouTube na ahadi yake ni kuwa ikifikisha views milioni 10 atatoa ngoma mpya.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news