TANZANIA: Izzo Bizness Kufuata Nyayo za Navy Kenzo

Baada ya Navy Kenzo kudondosha albamu yao mapema mwaka huu, rapper Izzo Bizness ameamua kufuata nyayo hizo.

Rapper huyo ambaye kwa sasa nafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Rafiki’, kupitia mtandao wa Instagram amethibitisha kuachia albamu yake mpya mwaka huu.

“Workin on my ALBUM it’s gonna be out this year,” ameandika Izzo kwenye mtandao huo.

Wasanii wengine ambao waliahidi kuachia albamu mwaka huu ni pamoja na Diamond, Vanessa Mdee, Fid Q, Roma na Stamina na wengine.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news