TANZANIA: Ommy Dimpoz Ataja Hasara za Kutoa Video Nyingi Kwa Wakati Mmoja

Msanii Ommy Dimpoz ametaja faida na hasara kwa msanii kutoa video nyingi kwa wakati mmoja.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya Cheche, ameiambia EA Radio iwapo msanii atatoa video nyingi moja wapo inaweza kufanikiwa na iwapo zote zikifeli atakuwa amejiondoa katika media rotation.

“Kila mtu ana biashara yake na anavyoingalia mipango yake ambayo anahisi inaweza kumsukuma, pengine anataka kuangalia katika hizi tatu ninazotoa moja haiwezi kukataa lakini kuna faida na hasara. Faida yake nyimbo zinaweza zikabahatika zikapenya zote kutokana na ukali wa nyimbo. Zikifeli zote itakuwa Stress coz umeshatumia gharama, umeshoot video za gharama halafu zote zimekataa kwa sababu hukuwekeza kwenye audio.

“Lakini pia mfumo wetu aina ulivyo unaweza ukajipoteza katika rotation kama msanii kwa sababu kwenye kipindi kimoja radio haiwezi kupiga nyimbo zako tatu, inaweza ikapigwa hii ikaua nyingine, kwa hiyo ni mchezo ambao inabidi uwe na mahesabu makali,” amesisitiza.

Mtindo wa msanii kutoa nyimbo au video nyingi kwa wakati mmoja ameanza kushika kasi katika Bongo Flava na mfano mzuri ni Diamond na Weusi ambao hivi karibuni wamefanya hivyo. Hata hivyo kuna baadhi ya watu wanapinga utaraibu huo na wengine wanaunga mkono.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news