KENYA: Walichosema Sauti Sol Kuhusu Snoop Dogg

May 25 mwaka huu rapper mwenye heshima kubwa nchini Marekani, Snoop Dogg katika mtandao wake wa Instagram aliweka video fupi ya kundi la Sauti Sol la nchini Kenya ikionyesha wakiperform mbele ya wanafunzi hit song yao ‘Leo Kuliko Jana’, sasa kundi hilo limefunguka machache kuhusu kitendo hicho.

Member wa kundi hilo Bien-aime baraza amekiambia kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen Kenya kuwa ni kitu ambacho hawakukitarajia kwani walishasahau wimbo huo na walikuwa katika mipango ya kufanya kitu kingine kikubwa zaidi.

“Ni Baraka sana tu halafu inaonyesha wakati mwingine kama msanii unakuwa haufikiri juu ya song, ni kama hiyo song ilishapita unataka usonge mbele na vitu vingine lakini Mungu anakubariki kwa ile kazi umekuwa ukiifanya, hivyo kazi inaendelea kujiendeleza.

Amesema na kuongeza kuwa, “so mazee tunasema asante pia kwa mashabiki wetu kwa kutuweka hizo level mpaka Snoop anatupata.

Sauti Sol ambao wameshafanya kazi na wasanii wa Tanzania kama AY na Alikiba, kwa sasa wametoa wimbo mpya ‘Friend Zone’.

Source. bongo5.com

Leave your comment

Other news