TANZANIA: Hii Ndio Sababu ya Nyimbo za Timbulo Kupendwa na Warembo

Msanii wa Bongo Fleva, Timbulo amesema ni kweli muziki wake umevuna mashabiki wengi kutoka kwenye kundi la warembo kutokana na tungo na muonekano wake pia.

Mwimbaji huyo ameeleza hata nyimbo zake za awali kama ‘Domo Langu’ zinapelekea hali hiyo na kuongeza hata baadhi ya wanaume wamekuwa wakipenda muziki wake lakini wamekuwa wagumu kuweka wazi hilo.

“Ni kweli si uongo kutokana na aina ya muziki ambao nimekuwa nikiufanya. Lakini kitu ambacho nakiamnini pia kwa upande wa pili mimi ni mmoja wa wasanii wakati nilivyoanza mwanzo washikaji wengi sana walitumia ngoma zangu kwa ajili ya kuwasilisha jumbe zao kwa watoto wa kike,” Timbulo amekiambia kipindi cha Show Time cha Radio RFA.

“Nikikurudisha nyuma kidogo unaweza kuona jinsi ngoma yangu ya Domo Zito ilivyoleta matokeo chanya na ilisababisha vijana wengi kuitwa Timbulo kwa kuwa niliimba sijui kutongoza. Hata kuna baadhi ya wadada waliwahi kunitumia, sometime unakuta mtu anakuelewa lakini anashindwa kukuambia,” ameongeza Timbulo.

Source: bonngo5.com

Leave your comment

Other news