TANZANIA: Ujumbe wa Jux Kwa Mpenzi Wake Vanessa Mdee Kwenye Birthday Yake

Mara nyingi mtu wako wa karibu anapokuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, ni muhimu kumpa ujumbe muhimu kuonyesha jinsi unavyomjali.

Jux ametumia vizuri nafasi hiyo katika siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake, Vanessa Mdee kwa kumwandikia ujumbe muhimu kupitia mtandao wa Instagram, unaoonyesha ni kiasi gani anamuheshimu na kumpenda mrembo wake huyo.

“Happy birthday #eastafricanqueen @vanessamdee more life n God bless you mama #bestfemaleartist #moneymondays,” ameandika Jux katika mtandao huo.

Couple ya wawili hao ambao wamekuwa katika mahusiano kwa takriban miaka miwili sasa, imeonekana kuwavutia watu wengi.

Source: bongo5.com

Leave your comment