TANZANIA: “Haikuwa Rahisi, Nilimchukua Jux Mpaka Kwa Bob Manecky” – Mimi Mars

 

Baada ya Shuga mwimbaji Mimi Mars ametuletea wimbo mpya ‘Dedee’ ambao umetayarishwa na Producer Bob Manecky na ameuzungumzia akisema haikuwa rahisi kufanya kazi na Manecky hivyo ilimlazimu amchukue Jux ili amsaidie kwenye wimbo huo.

Ayo TV na millardayo.com zimekutana na Mimi Mars ambaye hakusita pia kuzungumzia support anayoipata kutoka kwa watangazaji wenzake akieleza pia connection alizozipata hasa kukutana na ma-producer wakubwa kitu kilichomfanya kuongeza juhudi katika kazi yake ya muziki akiahidi kuendelea kutangaza na kuimba.

 

Source: millardayo.com

Leave your comment

Other news