TANZANIA: Nay Amtambulisha Msanii wa Kwanza wa Label Yake

Label ya ‘Free Nation 966’ ya rapa Nay wa Mitego imemtambulisha msanii wake wa kwanza aitwae ‘B Gway’. Rapa huyo amedai huyo ni msanii wake wa kwanza wa kurap kwani siku chache zijazo atamtambulisha msanii wake wa kuimba.

Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Nay amedai msanii huyo ataachia wimbo wake wa kwanza uitwao ‘Sijachukia’ ambao umetayarishwa na Yogo Beat.

“Leo label yangu ya ‘Free Nation 966’ imemtambulisha kijana wake wa kwanza ‘B Gway’,” alisema Nay. “Ni msanii mkali sana, sikutaka kumchukua msanii ambaye anatanisumbua, tena wimbo wake wa kwanza ‘Sijachukua’ amenishirikisha,”

Aliongeza, “Kwa hiyo ningependa kuwaambia mashabiki wasubirie mambo mazuri kutoka ‘Free Nation 966’. Pia siku chache zijazo tutamtangaza msanii mwingine wa kuimba,”

Wimbo wa msanii huyo kuachiwa Jumatano hii kupitia redio na runinga pamoja na mitandaoni.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news