Lil Wayne Ajiunga na Roc Nation ya Jay Z

Tayari Lil Wayne alishamalizana na Roc Nation ya Jay Z – na yeye ni mmoja ya wasanii wa familia hiyo.

Rapper huyo amethibitisha hilo tena kwa mara ya pili katika show ya Slippery Rock University huko Pennsylvania. “It’s the Roc! You know I’m a member of that team now,” amesema Wayne kwenye tamasha hilo.

Mwezi Novemba mwaka jana katika moja ya show za Drake nchini Marekani, Lil Wayne alipanda jukwaani na kuonyesha kuwa ni mmoja wa wasanii wa Roc Nation lakini kauli hiyo haikuwashtua mashabiki huku wakifikiria ni utani kutoka kwa rapper huyo.

“I’m a motherfuckin’ R-O-C millionaire. I’m a motherfuckin’ Roc-a-Fella millionaire,” alisema Weezy.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news