TANZANIA: Kufanya Hip-hop Kwa Mtoto wa Kike Kuna Mitihani Mizito - Tammy The Baddest

Tammy The Baddest amedai kuwa kufanya hip hop kwa rapper wa kike kuna mitihani mingi.

Ameiambia Bongo5 kuwa kwa upande wake awali ilikuwa ngumu zaidi kueleweka kwasababu anatoka kwenye familia ya kiislamu. “Wanaamini kwamba mtoto wa kike ukimaliza shule, ukimaliza chuo ukianza kupata mabadiliko ya kike inabidi uolewe,” anasema Tammy. “And for me to convince my family kwamba mimi nafanya hip hop unaweza ukaelewa mwenyewe, sio kitu rahisi,” ameongeza.

Tammy amedai kuwa changamoto nyingine kubwa ni wadau wa muziki kutotoa support kwa rappers wa kike kama wanavyotoa kwa wenzao wa kiume.

“Kibongobongo hakuna kabisa,” anasema. “Mimi nakumbuka nilipelekwa na kaka yangu mmoja hivi wa hip hop kwa mtu ambaye alisema atanisaidia anapenda rap, nikamsikilizisha ngoma zangu akaniambia ‘lakini una kitu, labda hautoki kwasababu ya huu muziki unaofanya, ungejaribu kufanya kama Shilole, for real? No offence to Shilole I love her, but for you to tell me nitoke kwenye hip hop nifanye muziki fulani ambao kwangu mimi sio kitu ninachopenda, ni kama unanitukana,” amesisitiza.

Tammy kwa sasa ana wimbo mpya uitwao Mtoto wa Kike.

Source: bongo5.com

Leave your comment