Kaka Yake Victoria Kimani, Kimya Azungumzia Mafanikio ya Dada Yao

Muimbaji wa Kenya aliyesainishwa na label ya Nigeria, Chocolate City, Victoria Kimani, alizaliwa kwenye familia yenye vipaji vya muziki.

Kaka zake wawili, Bamboo na Kimya, ni miongoni mwa rappers wanaoheshimika zaidi Afrika Mashariki. Wiki hii Kimya ambaye jina lake halisi ni Clarence Kimani, ametutembelea kwenye studio zetu na kumuuliza anazungumziaje mafanikio ya dada yao Victoria.

“I am so proud of her, kusema ukweli she is the best in the family,” anasema.

“Ameweza kufanya makubwa sana and she is continuing to do it and nilikuwa nawaambia jamaa juzi wakacheka, when she was young alikuwa anaimba nyumbani na mimi na Bamboo tunamwambia anyamaze ‘we acha kupiga kelele, unafikiria wewe ni Beyonce’, alikuwa anaimba kwa hisia sisi tunaona hii ni kero as big brothers. But we never knew what her talent is and what her passion in life will be, she has done it so well and she is continuing, na tena amefanya kazi na watu wengi sana Afrika hii.”

Kimya amesema watatu pamoja wamefanya nyimbo kadhaa na wataendelea kurekodi.

Victoria ana album mpya iitwayo Safari

Akizungumzia kwanini Victoria Kiswahili kinamshinda, Kimya amedai kuwa dada yao hakuwahi kuishi Kenya kwa muda mrefu kama wao. Anasema maisha yake mengi akiwa mdogo yalikuwa ni Marekani na Nigeria ambako baba yake alikuwa akifanya kazi kama mchunguji na hivyo kukosa wasaa wa kuzungumza Kiswahili kama kaka zake.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news