TANZANIA: Profesa Jay Ataja Jina la Albamu Yake Ijayo, Afunguka Kuhusu Harmorapa

Rapper mkongwe nchini Profesa Jay amefunguka kwa kutaja jina la albamu yake itakayokuja pamoja na kumzungumzia Harmorapa ambaye kwa sasa amekuwa akiteka vichwa vya habari.

Akiongea na kipindi cha Twenzetu cha Times FM Jumatano hii, Jay amesema amepanga kuachia albamu yake mpya ambayo itajulikana kama ‘The Icon’.

“Nimepanga kuja na albamu. Mimi niliahidi kutoa albamu toka kitambo ila sasa niko busy tu kutokana na majukumu ya hapa na pale ila nimejipanga kutoa albamu mpya na itaitwa ‘The Icon’ kama ilivyo kwenye cover ya ngoma yangu mpya ‘Kibabe’ na nyingine zitakazo kuja,” amesema rapper huyo.

Wakati huo huo hitmaker huyo wa Kibabe, amemuongelea Harmorapa kwa kusema, “Watu wasishangae kumuona Harmorapa akifika mbali maana kila msanii anapitia hustle na yeye anahustle. Hivyo kufika mbali ni lengo la kila msanii na mimi napenda kumheshimu kila msanii kutokana na jitihada zake.”

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news