TANZANIA: Nawathamini Mashabiki Zangu wa Kenya Kuliko Hela - Darassa

Wakati wimbo wake ‘Muziki’ ukiendelea kufanya vizuri katika chati zote za redio na TV mbali mbali na pia mitaani kwetu Kenya, ambako ngoma hiyo inaimbwa na watu wa rika lote na kuchezeshwa kwenye mabodaboda na madaladala, rapper huyu amedhihirisha kwamba ni kweli hamna yeyote anayeweza kukwamisha riziki ya mwenzake, labda kuichelewesha.

Mkali huyu alikuwa na ujumbe maalum kwa mashabiki zake wote wa Kenya. Alizungumza time fulani na mtangazaji maridadi, Dickson Stanley wa kituo cha Sunrise radio (Arusha) kwenye kipindi cha Fleva Plus na kusema yote ya moyoni.

Aliulizwa ni kwanini hajaenda Kenya kupiga shows za kumuingizia hela kibao wakati huu ambapo wengi wana kiu ya kumwona akiperform pande hizo naye akajibu: Kenya…mimi nafikiri kuna watu wangu wengi kuliko hela. So I don’t see hata nikienda hela inakuwa tu part ya maisha yangu, lazima niishi nayo siwezi kuacha. Lakini siweki hela kwenye thamani ambayo pengine dunia imeipa. Sitaki hela ziingilie thamani ya watu, sitaki hela ikae katikati ya mtu na mtu,” alisema Darassa.

“So hela ni part ya kuendesha vitu vyetu vya kila siku. Lakini hela haziwezi kuwa thamani yako wewe, kuchagua thamani ya hela mbele yako, siwezi kuwa mtu ambaye anataka kuwa. So respect ambayo ninayo Kenya watu wanatusupport kazi zetu na wanatuhitaji. Tunahitajika karibu dunia nzima ambako muziki wetu unafika na tuna utaratibu wa kufika hapo.”

Source: bongo5.com

Leave your comment