TANZANIA: Mwanamke Inatakiwa Uanze Kujitambua Mwenyewe – Christina Shusho

Msanii wa muziki wa Injili, Christina Shusho amewataka wanawake kujithamini na kujituma katika kazi ili waweze kutambuliwa na watu wengine katika jamii.

Shusho ameiambia TBC1 kuwa mwanamke hukutana na changamoto nyingi lakini akijitambua na kujithamini atashinda changamoto hizo.

Alisema, “Mwananmke anatakiwa apewe na nafasi na baada ya kupewa nafasi inatakiwa aanze kujitambua yeye mwenyewe, aanze kujipa nafasi, aanze kuonesha kile anachokiweza kabla ya mtu mwingine hajamuamini kumpa nafasi, so to raise our standard.”

Aliongeza, “Mama ni mtu mzuri sana, mama ajitambue na awe tayari kwa nafasi atakayokuwa nayo na aifanye kwa uaminifu,aibu ndogondogo hizi lazima tuwe tunaziondoa kwa upande wa wanawake tufute.”

By: Na Emmy Mwaipopo (bongo5.com)

Leave your comment

Other news