TANZANIA: Industry Ndiyo Inapelekea Wasanii Kuachia Nyimbo Nyingi Kwa Muda Mfupi - Nick wa Pili

Nick wa Pili amefunguka sababu inayofanya wasanii kuachia nyimbo nyingi baada ya muda mfupi.

Rapper huyo amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One, industry ndiyo inapelekea wasanii kuachia nyimbo nyingi.

“Nyimbo sasa hivi hazidumu muda mrefu kwa sababu ukiangalia industry yenyewe inavyoenda imebase kupiga kazi mpya. Kwahiyo unakuta sasa hivi nyimbo inatoka miezi mitatu inafifia,” amesema Nikki.

“Industry imechukua mtizamo wa kucheza nyimbo mpya na mashabiki nao wamezoeshwa hivyo kwa hiyo muziki umekuwa kama bidhaa sokoni ambazo zinabidi ziingie na kutoka ili bidhaa zingine ziingie. Kwahiyo tunapoelekea msanii anatakiwa atoe nyimbo nyingi sana kwa mwaka , itafikia mtu anatakiwa atoe hits tanoi labda kwa mwaka,” ameongeza.

Source: bongo5.com

Leave your comment

Other news