TANZANIA: Wasanii Hawa Waungana Kumsaidia Jetman

Wasanii watatu wa bongo fleva wameungana na wadau wengine katika kampeni ya 'Amka na Jet Man' kwa lengo la kumsaidia msanii mwenzao kutoka Jiji la Mwanza aliyepatwa matatizo ya kupooza mgongo na kumsababishia kulala kitandani takribani miaka 4 sasa.

Wasanii hao ni Ben Pol, Barakah The Prince na Jux ambao ni miongoni mwa wasanii walioweza kununua vionjo hivyo kwa kiasi cha shilingi laki moja kwa kila mmoja na kutoa mchango wao wa jumla wa shilingi laki 5.

“Katika fedha tulizoingiza tumetoa Sh 500,000 na pia tumeongeza kila mmoja Sh 100,000, imefika Sh 800,000 tumempa rafiki yetu na msanii mwenzetu kwa mapenzi yetu ili zimsaidie katika baadhi ya mahitaji yake’’. Alisema Ben Pol 

Aidha msanii huyo alisema huo siyo mwisho wao wa kumsaidia rafiki yao watazidi kutoa kwa kile walichojaaliwa kadri ya uwezo wao.

Jetman

Licha ya maumivu makali anayoyapata msanii huyo hajaacha kufanya muziki sababu anaamini ndio mkombozi wake,wasanii wengi wameonekana kuguswa na suala hilo wengine wakipendekeza 'Riddim' za nyimbo zake ziuzwe ili waweze kupata kiasi cha shilingi milioni 12 aweze kwenda nchini India kupatiwa matibabu.  

Source: eatv.tv

Leave your comment

Other news