TANZANIA: Ben Pol Apiga Chini Kutoa Album, Adai Mbioni Kuja Na EP ‘Extended Play’

Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol amesema kuwa hatotoa Album mwaka huu au mwakani ila anatarajia kutoa EP (nyimbo chache zinazo unganishwa pamoja) ambayo itakuwa na nyimbo 7 ambazo hazijawahi kusikika popote.

Ben Pol amedai kuwa kwenye EP hiyo ambayo ataitoa mwaka huu kutakuwa na nyimbo aliyerekodi na Chiddima kutoka Nigeria.

“Sidhani kama nitatoa album ila nitatoa EP ambayo itakuwa na nyimbo 7 ambazo hazija wahi kusikika popote pale hapa nchini maana watu wasifikilie kuwa watasikia phone au moyo mashine na nitaitoa ndani ya mwaka huu” Alisema Ben Pol kwenye kipindi cha Twenzetu cha TimesFm.

Instagram photo by BEN POL _MzeeBaba_BPaTQ4Ehwso - JPGBen Pol

Mbali na hilo Ben pia alidai anatamani sana kuwasaida baadhi ya wasanii ambao wapo level za chini na anatamani kuwapush ili wafike level za juu zaidi kwenye Game hapa bongo.

Ben Pol aliwataja Ibrah Nation, Foby, Ivra kuwa ni kati ya wasanii ambao anatamani kuwasaida ili kuwavusha kwenye level za juu zaidi.

“Unajua huwezi kusema wazi kuwa unataka kumsaida mtu fulani maana sio kila mktu anahitaji msaada kama unavyodhani ila mimi nadhani kama ni kuwasaida basi ningewasani Ibrah Nation, Ivra na jamaa mmoja hivi kaimba nyimbo ya mimi ni staa nadhani anaitwa Foby so nadhani hao ndio niotamani sana uwasaidia” Alisema Ben Pol.

Aidha Ben Pol ameweka wazi kuwa Rapa Hamorapa alimpigia simu wiki mbili zilizopita so kitu chochote kinaweza kutokea.

Source: perfect255.com

Leave your comment

Other news