TANZANIA: Fid Q Akaribia Kuachia Kitabu Chake Cha Kwanza ‘The Swahili Kid’

Mbali na kuwa na misemo migumu ya kumfanya mtu kutumia muda mwingi kusikiliza kwa umakini mashairi ya nyimbo zake, sasa rapper Fid Q ameingia kwenye uandishi wa vitabu.

Rapper huyo ameiambia Bongo5, kitabu chake hicho cha kwanza kinaitwa ‘The Swahili Kid’ na kitatoka baada ya albamu yake ya tatu Kitaaolojia.

“Nina kitabu kizima ambacho kinakuja kinaitwa ‘The Swahili Kid’. Ambacho kinasubiriwa kama inavyosubiriwa albamu yangu ya tatu ‘Kitaaolojia’. Kwenye kitabu hicho nimechambua kuanzia albamu yangu ya kwanza, ya pili na mpaka hii ya tatu. Kinachelewa kutoka kwa sababu sasa hivi nipo kwenye albamu yangu ya tatu ‘Kitaaolojia’,” amesema Fid.

Rapper huyo ameongeza kitabu hicho kitatoka pindi albamu yake hiyo ya tatu itakapotoka Agosti 13 ya mwaka huu.

Source: bongo5.com

Leave your comment