TANZANIA: Ukiimba mapenzi ndiyo watu wanakuwa wepesi ku-catch tofauti na ukiimba vitu vingine – Belle 9

 

 

Msanii wa Bongo Fleva, Belle 9 amefunguka sababu za yeye pamoja na wasanii wengi wa muziki huo kuimba nyimbo zenye ujumbe wa mapenzi zaidi ya ujumbe mwingine. Belle 9 akijibu maswali ya mashabiki na wapenzi wa muziki kupitia Kikaangoni ya EATV amesema sababu kubwa ya yeye kutunga nyimbo za aina hiyo ni biashara kwa kuwa ujumbe huo ndiyo unaopendwa zaidi na mashabiki wa muziki.


“Tunaimba mapenzi kwa sababu za kibiashara, ukiimba mapenzi ndiyo watu wanakuwa wepesi ku-catch tofauti na ukiimba vitu vingine, kwahiyo tunaimba mapenzi kwa sababu za kibiashara kwa kuwa watu ndiyo wanapenda". Alisema Belle 9.


Nyimbo nyingi ambazo ameimba Bell 9 na zika-'hit' zilikuwa na ujumbe wa mapenzi isipokuwa ule wa 'Nilipe Nisepe' ambao ulikuwa na ujumbe tofauti kabisa.
Baadhi ya nyimbo hizo ni kama vile Sumu ya Penzi (uliomtoa), Masogange, Burger Movie Selfie, Shauri Zao, Listen na ngoma yake mpya aliyoita vionjo vya Saida Karoli, 'Givi it to me'.
Akijibu swali kuhusu mafanikio aliyoyapa hadi sasa katika muziki, Belle 9 alisema "Kuna mafanikio mengi nimeyapata, kubwa ikiwa ni kipato, lakini nimeongeza watu, najitegemea, sitegemei tena mtu"


Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment