TANZANIA: Ben Pol awachana wanaoichukia #Muziki

 

 

Mwanamuziki Ben Pol ambaye ameshirikishwa katika wimbo wa Darassa 'Muziki' amefunguka na kuonesha kushangaa watu zaidi ya elfu mbili ambao wameonesha kutopendezwa na wimbo wa Darassa.

Ben Pol alitumia mitandao yake ya jamii kuonesha kuwa hata ukifanya jambo kubwa na zuri ambalo linaweza kuwafurahisha watu wengi zaidi lakini wapo watu ambao watatokea na kukukatisha tamaa, kukuvunja moyo hivyo siku zote usivunjike moyo na maneno ya watu bali inatakiwa usimamie kile unachokiamini kwani ni vigumu sana kumfurahisha kila mtu katika dunia hii.

"Pamoja na kuvunja rekodi na pia mafanikio ambayo wimbo huu 'Muziki' umeleta na unaendelea kuleta, Eti kuna watu buku mbili hawakuuelewa, hapo ndiyo utaamini kwamba haiwezekani kuwafurahisha watu wote duniani, lazima atatokea/Watatokea vichwa ngumu kadhaa tu ambao hawatakuelewa unachofanya, focus, Stick to your plans, Move forward, Conquer" aliandika Ben Pol.

 

 

Unaweza kutazama hapa video hiyo ya #muziki:

 

Leave your comment