TANZANIA: Nimechoshwa kuzungushwa – Young Killer

 

 

Msanii wa hip hop nchini Young Killer amezungumzia 'bifu' kati yake na aliyekuwa meneja wake Monagangster na kusema kuwa hataki tena kufuatilia malipo katika kazi ambazo alizifanya akiwa na meneja wake huyo.

Amezungumza hayo alipokutana na Kamera ya eNewz na kusema kwa sasa hataki tena kufuatilia pesa kwa sababu ameona kama anazungushwa sana na sasa amechoka.

“Ni kwamba nimechoka kuzungushwa na ndiyo maana sasa hivi nimeona nifanye kazi zangu nyingine ambazo naamini zinaweza zikaniingizia mkwanja mrefu kuliko hata huo”

Pia alizungumzia kuhusu tetesi za kuwa tangu ameacha kufanya kazi na meneja wake huyo nyimbo ambazo amekuwa akizitoa zimekuwa hazifanyi vizuri. Amekanusha hilo na kusema ameweza kutoa ngoma nyingi na zote zinafanya vizuri, ikiwemo Popote Kambi ambayo amemshirikisha Juma Nature.

“Mimi sidhani kama ni kweli, kuna ngoma ambazo nimezitoa na zimefanya vizuri kama Popote Kambi, Kumi na Tatu. Zote zimefanya vizuri kwa hiyo hayo yanayosemwa sio ya kweli”

Young Killer mwanzoni alikuwa akifanya kazi na Monagangster ambaye alikuwa akimsimamia kwenye kazi zake kama vile Mrs Superstar na nyingine nyingi lakini hapo baadaye Young Killer alijitoa kwake kwa Mona na kuanza kufanya kazi zake mwenyewe bila usimamizi

Leave your comment

Other news