TANZANIA: Darasa afunguka juu ya mitazamo ya mashabiki kumtaja kuwa rapa namba 1 kwa sasa

 

 

 

Rapper anayefanya vizuri kwa sasa kwenye muziki wa Hip Hop, Darassa amefunguka juu ya mtazamo wa mashabiki na wadau mbalimbali kumtaja kama ndio rapper namba moja kwa sasa nchini.

Darassa amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One, “Sikuwa nimeplan hivyo lakini naona watu wanaweka huo mtazamo kwa sasa kutokana na hard work niliyoionyesha na still nipo bado nipo kwenye changamoto ya kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha nafikia malengo yangu. Lengo langu si kuamka asubuhi watu wakasema mimi ndio best rapper au mimi ninaweza kuwa mkali kwenye hiki kipindi lengo langu ni kuweka historia kwenye muziki wangu hata kama nisipotoa wimbo historia yangu ibaki inafanya kazi. Naomba Mungu anisaidie sana kwa hili.”

“Nafikiri Too Much inahitaji wimbo mwingine kwa sababu toka nimeutoa hakuna wimbo mwingine unaweza kukaa juu ya wimbo huo. So hakuna sababu ya sisi kuendelea kusubiri mashabiki wetu wanahitaji burudani, ndio sababu kubwa imepelekea kuleta project hii mpya.”

Rapper huyo ameongeza kuwa wimbo wake mpya wa ‘Muziki’ ambao mpaka sasa umetazamwa zaidi ya mara 801k kwenye mtandao wa Youtube umetayarishwa na maproducer watatu akiwemo Mr VS, Mr T-Touch na Abbah wa Abbah Process

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news