TANZANIA: Seline aelezea sababu ya kujitoa The Industry

 
 
 
 
May 6 mwaka huu, label ya The Industry inayomilikiwa na Nahreel na Aika (Navy Kenzo) iliwatambulisha wasanii wake watatu, Rosa Ree, Seline na Wildad.
Baada tu ya kuwatambulisha, walianza kwa kuachia kazi ya Seline iliyoitwa Njoo. Na wiki hii, kazi za wasanii wawili, Rosa Ree na Wildad zimetambulishwa lakini uongozi wa The Industry ukatangaza kuwa Seline hayupo nao tena.

“Tahadhari kutoka uongozi wa The Industry Studios Tanzania, msanii Seline (Roseline Muhagachi) hayupo tena chini ya uongozi wa Lebo ya The Industry inayomilikiwa na Navykenzo (Aika na Nahreel),” ilisema taarifa hiyo.
 
 
“Hii ni kutokana na matukio mbali mbali ya utovu wa nidhamu ambayo yalitokea akiwa chini ya uongozi wa Lebo hiyo. The Industry Studios haihusiki na shughuli,matangazo wala matukio yoyote yanayomuhusu mwanadada Roseline Muhagachi anayejulikana kwa jina la kisanii Seline,” yaliongeza.
Bongo5 imezungumza na Seline kutaka kujua upande wake ukoje na kama tuhuma za nidhamu ni za kweli. Seline ana hadithi tofauti huku akikanusha kuonesha utovu wa nidhamu na kwamba ni yeye ndiye aliyejiondoa.

“There is a very sad story behind all of that,” anasema.“Halafu mimi nimejitoa The Industry mwenyewe hakuna aliyeniondoa pale. Nilienda kuinvest hela yangu pale, a lot of money, and hawakufanya kazi wanayopaswa kufanya,” ameongeza.
 
“I am a professional, nimefanya kazi hadi na government za nchi nyingine, kweli leo nitolewe kwenye studio kisa misconduct?” “Kifupi I invested my money kwao and they didn’t work on our terms and many more factors behind it,” amesisitiza.
 
Kwa sasa Seline anatamba na kibao chake cha 'Dollar', tazama hapa video yake:


Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

 

Leave your comment

Other news